Kocha wa mabingwa wa soka duniani timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps, amewalaumu wachezaji wake kwa kushinda kufikia lengo la kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Ujerumani, katika mchezo wa michuano ya ligi ya mataifa ya Ulaya (UEFA Nations Leagua) uliocheza usiku wa kuamkia leo.
Miamba hiyo ya soka ilikutana mjini Munich katika mchezo wa kundi A wa michuano hiyo, inayofanyika kwa mara ya kwanza barani Ulaya na kushuhudia ikishindwa kufungana.
Kocha Deschamps aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo huo kuwa, kikosi chake kilifanya makosa mengi ambayo yamewakosesha ushindi katika uwanja wa ugenini.
Alisema aliweka mipango mizuri kabla na wakati wa mapumziko ambayo aanaamini kama ingetumika vizuri, Ufaransa huenda wangeondoka ugenini na ushindi mzuri wa mabao.
“Sikupendezwa na walivyocheza, wameonyesha udhaifu mkubwa dhidi ya wapinzani wetu, hatukupaswa kupata matokeo ya bila kufungana,” Alisema kocha huyo mwenye umri wamiaka 49.
“Hawakufuata maelekezo niliyowapa kabla na wakati wa mapumziko, niliamini wangefanikisha hilo, lakini ilikua tofauti kabisa, matokeo yake tumeopata alama moja.”
“Lengo letu kubwa lilikua ni kupata ushindi katika mchezo huu ili tujiweke katika mazingira ya kuongoza msimamo wa kundi letu, lakini hatuna budi kukubaliana na matokeo yaliyopatikana, tutajipanga kwa mchezo unaofuata.”
Mchezo wa jana dhidi ya Ujerumani ulikuwa wa kwanza kwa kocha Deschamps baada ya kukamilisha jukumu la kutwaa ubingwa wa dunia nchini Urusi, kwa kuichapa Croatia mabao manne kwa mawili mwezi Julai.
Ufaransa watacheza mchezo wa mzunguuko wa pili wa kundi A Septemba 09, dhidi ya Uholanzi kwenye uwanja wa taifa mjini Paris (Stade de France).
Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mataifa ya Ulaya (UEFA Nationas League).
Kundi B
Jamuhiri ya Czech 1 – 2 Ukraine
Wales 4 – 1 Ireland
Kundi C
Norway 2 – 0 Cyprus
Slovenia 1 – 2 Bulgaria
Kundi D
Kazakhstan 0 – 2 Georgia
Latvia 0 – 0 Andorra
Kundi E.
Armenia2 – 1Liechtenstein
Gibraltar 0 – 2 FYR Macedonia
Michuano hiyo itaendelea tena hii leo .
Kundi A
Italy Vs Poland
Kundi B
Turkey Vs Russia
Kundi C
Albania Vs Israel
Lithuania Vs Serbia
Romania Vs Montenegro
Kundi D
Azerbaijan Vs Kosovo
Faroe Islands Vs Malta