Wachezaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Feisal Salim, Aziz Ki na Fiston Mayele wametajwa kuwa miongoni mwa watakaoshiriki kwenye kampeni ya mtaa kwa mtaa ya klabu hiyo kwa ajili ya kuhamasisha watu kuchanja na kupata elimu ya kujilinda na Uviko 19 na Ebola.

Wengine waliotajwa ni Dickson Job, huku kampeni hiyo ikitarajiwa kufanyika kwa siku tano kuanzia kesho hadi Novemba 2 kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Club Africain ya Tunisia wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Afisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe amesema klabu imebeba jukumu hilo ikishirikiana na UNICEF na Jackson Group.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Jackson Group, Kelvin Twisa amefafanua kwamba wakati shughuli hiyo ikiendelea, wachezaji watakuwa wakiendelea pia na programu za kocha kwa ajili ya mechi hiyo.

Amesema kampeni hiyo mbali na elimu, pia itahamasisha watu kuchanja.

“Klabu itatoa tiketi 10,000, kwa watu watakaoelimika na kuchanja katika kampeni hii,” amesema na kuongeza

“Mbali na elimu na kuchanja, tutatoa zawadi za jezi, kofia na mashabiki kuwa karibu na makombe yetu yote matatu na kupiga nayo picha,’

Akizungumzia tukio hilo, Mtendaji Mkuu wa Young Africans, Anore Mtime amesema walisaini mkataba na UNICEF kutoa elimu ya Uviko 19 na ebola na kampeni hiyo inaanza kesho.

Rais ataka changamoto za kitaasisi zishughulikiwe
Mwakinyo aporokoma nafasi mbili, Kidunda apaa