Kocha Mkuu wa Kikosi cha Young Africans Nasreddine Nabi, amesema ni muhimu wachezaji kuwa na mwendelezo wa nidhamu kwenye michezo yote inayowakabili ili kupunguza makosa ya kufungwa.

Timu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 68 baada ya kucheza michezo 26, huku leo Alhamis (Mei 04) ikitarajiwa kumenyana na Singida Big Stars kwenye Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida.

Kocha Nabi amesema kazi kubwa ya wachezaji ni kutafuta ushindi na kucheza kwa nidhamu ili kupata matokeo mazuri.

“Mchezo wa mpira unahitaji nidhamu, hivyo wachezaji ni muhimu kuendeleza nidhamu kwenye kukaba na kupunguza makosa kwani mpira ni mchezo wa makosa ukikosea unaweza kuadhibiwa.”

“Ninawapongeza kwa kazi ambayo wanafanya uwanjani bado kazi inabidi kuendelea kufanyika mpaka mwisho kwani kila mechi ina ushindani wake na mbinu zake, kikubwa ni kuona tunashinda,” amesema Kocha huyo kutoka Tunisia

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizo zilipokutana Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Young Africans iliifumua Singida Big Stars 4-1, na kuvuna alama zote tatu.

Hans van Pluijm: Tunaiheshimu Young Africans
Mkakati chumba maalum kunusuru ndoa waleta mafanikio