Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanafunzi wa darasa la saba kuepuka udanganyifu katika mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.
Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 baada ya kukagua ujenzi wa shule ya mfano inayojengwa katika kata ya Iyumbu jijini Dodoma.
Profesa Ndalichako amesema maandalizi ya mitihani hiyo imekamilika na vifaa pamoja na mitihani imeshasambazwa kwenye vitu
“Miaka miwili mitatu iliyopita kumeanza kuwa na vidalili dalili vya kuijaribu Serikali watu wamekuwa wakifanya udanganyifu katika mitihani. Naomba niwatadharishe kuwa Serikali iko imara na tutakuwa makini katika kuhakikisha mitihani inafanyika kwa kuzingatia taratibu,”amesema.
Amesema yeyote atakayeshulika na vitendo vya udanganyifu Serikali itachukua hatua kwa mujibu wa taratibu.
Wanafunzi hao wanatarajia kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi Septemba 8 hadi 9 mwaka huu ikiwa ni awamu ya kwanza tangu utaratibu wa elimu bila malipo uanze nchini.