Baadhi ya Wadau wa Habari, wamepongeza kauli ya Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa, Prof. Rwekaza Mukandala cha kutaka Wanahabari waunde chombo cha kusimamia maadili yao na vyombo vyao vya Habari.

Prof. Mukandala aliyasema hayo hivi karibuni (Oktoba 21, 2022) wakati akiwasilisha taarifa ya Kikosi kazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan maoni ya Wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mbali na kuunda chombo hicho, pia Prof. Mukandala alipendekeza uwekwe utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa sheria husika katika pendekezo la 17 la Kikosi kuhusi uhusiano wa mawasiliano kwa umma, vyombo vya habari na siasa.

Rais Samia akipokea taarifa ya kikosi kazi.

Wadau hao wamesema, uwepo wa chombo hicho utasaidi kupunguza ukakasi uliopo na kwamba nyakati zimefika za kuungana na baadhi ya Mataifa kuleta uhuru kwa Wanahabari kufanya kazi zao bila hofu, kitu kitakachosaidia ufanisi na utekelezaji wa majukumu yao.

Mmoja wa Wadau hao, Jimmy Ladislaus amesema suala la mabadiliko ya sheria za habari kwasasa halipingiki na wakati umefika kwani wamekuwa wakilipigania siku zote na tayari serikali imeanza mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari yam waka 2016 kitu ambacho kinaleta mwanga.

Katika mapendekezo la Kikosi kazi, pia Mwenyekiti huyo pia alisema vyombo vya Habari vya umma vipewe fursa sawa kutangaza habari za wagombea wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi bila upendeleo.

Waziri Mkuu apewa tahadhari ukali wa maisha
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 23, 2022