Bara la Afrika linajulikana ulimwenguni kwa sifa nyingi ikiwemo utajiri wa rasilimali, umaskini, ukosefu wa usalama na ufisadi, jambo ambalo limefanya baadhi ya maeno kuwa maarufu kulingana na sifa mojawapo kati ya hizo chache zilizo orodheshwa.

Na kwa miaka mingi, viongozi wa Kiafrika wamekuwa wakiwakatisha tamaa zaidi wananchi wao kwani baadhi yao huanza vizuri katikia kuwaongoza na kushughuilikia matatizo ya Wananchi lakini baadaye hushindwa kuendeleza kasi waliyoanza nayo.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa Afrika wametofautiana kimtazamo na hata kimaamuzi na Viongozi wengine kutokana na huduma zao za kujitolea kwa watu wao jamii nzima inayowazunguka ili kuhakikisha kwamba watu wao wanakuwa huru na huru kujieleza.

Si hivyo tu, pia baadhi ya Viongozi walileta maendeleo katika nchi zao na matokeo yake, wakaandika majina yao katika historia ambayo mpaka leo hii mataifa husika yana

endelea kujivunia mbele ya umati na kimataifa juu ya mema yaliyoachwa na Viongozi hao.

Nimekuandalia Wasifu mfupi wa Viongozi wakuu katika bara la Afrika ambao kwa nyakati tofauti wakati wa uongozi wao waliweza kufanya mambo makubwa yaliyoacha alama za kihistoria kwa vizazi vya sasa na vya baadaye.

  1. Nelson Mandela

Alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, lakini kabla ya kuwa rais alipigana dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na kujitolea sehemu ya maisha yake ya utu uzima kukaa gerezani.

Alitumikia kifungo cha miaka 27 kutokana na harakati zake za mapinduzi na baada ya kuachiliwa huru, chama chake cha African National Congress – ANC, kilishinda uchaguzi mkuu wa mwaka 1994, unaoelezewa kuwa ni uchaguzi wa kwanza uliokuwa huru na wa haki nchini Afrika Kusini katika historia.

Nelson Mandela almaarufu ‘Madiba’ kama alivyoitwa na wafuasi wake kwa furaha, alikua ni Rais mwenye utu wa pekee na aliwasamehe maadui zake wote kwa kuunda tume ya maridhiano, ambayo Askofu Mkuu wa Anglikana, Desmond Tutu aliongoza.

Alichukizwa na ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi na chini ya uongozi wake ubaguzi wa rangi ulimalizika nchini Afrika Kusini na kukawepo na ushirikiano wa mafanikio kati ya wazungu na weusi.

Wazee wanasema “Kichwa kinachosinzia kinahitaji shingo ya ziada ili kisipinde au kuinama”. Ukisinzia ni vigumu kichwa kubaki kimenyooka kitapinda au kuinama na hapo tunajifunza kitu kuwa tunahitaji usaidizi.

Kila kiongozi anahitaji msaada wa karibu kwani akitegemea nguvu zake mwenyewe bila kukubali kusaidiwa mambo mengi yatapinda au kuinama, na katika hili Nelson Mandela alifaulu kwani hakukumbatia madaraka bali alishirikiana vyema na watu nje na ndani akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika kufanikisha uhuru wa Taifa la Afrika Kusini.

Hatimaye Mandela akashinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1993, kwa kuleta amani nchini Afrika Kusini kupitia miradi yake, iliyomaliza miongo kadhaa ya kikatili ya ubaguzi wa rangi.

Itaendelea………..

Harry Kane: Spurs inapaswa kushiriki kimataifa
Kocha Simba SC aomba radhi, kukutana na uongozi