Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Hamisi Sudi amepiga marufuku uingizwaji wa bidhaa za vyakula ambazo hazijadhibitishwa na wataalamu wa Ubora kwenye masoko ili kumlinda mwananchi dhidi ya madhara.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wawekezaji pamoja na wajasiriamali wa bidhaa za vyakula mikoa ya kanda ya ziwa.
Aidha amewataka wawekezaji kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuleta ushindani wa kibiashara ukanda wa Afrika mashariki.
Naye Mkuu wa wilaya ya Geita, Fadhili Juma amewataka wananchi kutoa ushirikiano na taarifa kwa watu wanaoingiza bidhaa zisizo na ubora.
Jafari Donge meneja wa kuhudumia viwanda vidogo Mkoa wa Geita amesema wameanza mpango maalumu kuwawezesha wawekezaji wazawa na wajasiriamali kutengeneza bidhaa zenye ubora.