Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema Wafugaji Nchini hawana budi kuwa mabalozi wazuri na kuungano mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi mazingira kwa kufanya shughuli za ufugaji wenye tija kwa maendeleo endelevu.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa Wiki ya Maonesho ya Ufugaji wenye Tija na Utunzaji wa Mazingira sanjari na kuzindua Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Amesema ufugaji endelevu usioathiri hifadhi ya mazingira utasaidia katika kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini, wahimiza wafugaji ambao wamepata ufadhili kutumia fursa ya Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mabdiliko ya Tabianchi (COP 28) kushiriki kikamilifu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo.

“Tuepuke migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo tunashuhudia ikitokea katika baadhi ya mikoa nchini husababisha kutoelewana kwa makundi haya mawili hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, na tuna wajibu
wa kulinda amani,” amesisitiza Dkt. Jafo.

Mkutano huo, unatarajiwa kufanyika Umoja wa Falme za Kiarabu – UAE Novemba 28 – Desemba 5, 2023 utakuwa ni adhimu na fursa ya kuitangaza Tanzania namna inavyofanya ufugaji rafiki, huku Jafo akitoa wito kwa CHAMAUTA kulitumia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC, kupata uelewa wa kanuni zinazosimamia mazingira.

Tanzania, Ujerumani kuboresha Makumbusho ya Majimaji
Vijana wajiriwe kwa utaalam si uzoefu: Kikwete