Serikali ya Iran imewaachia huru wafungwa zaidi ya 54,000 ikiwa ni sehemu ya juhudi ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya jela.

Msemaji wa Mahakama, Gholamhossein Esmaili amewaambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao waliachiwa huru baada ya kupimwa na kukutwa wakiwa hawajaathirika na virusi hivyo.

Hata hivyo, Esmaili alieleza kuwa msamaha huo wa dharura hautawahusu wafungwa ambao wanatumikia vifungo vya zaidi ya miaka mitano jela.

Mfungwa ambaye ni raia wa Iran, Nazanin Zaghari-Ratcliffe naye yuko kwenye mpango wa kuachiliwa. Familia yake imekuwa ikilalamika kuwa amekataliwa kupimwa ingawa anaonesha kuwa ana dalili za maambukizi.

BBC imeeleza kuwa Mbunge wa Uingereza anaweza kuachiwa huru wiki hii kutokana na hali yake ilivyo. Alikamatwa na kuhumiwa kwenda jela kwa makosa ya kudukua taarifa za siri za Iran.

Watu 90,000 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya Corona aina ya Covid-19 duniani kote na vifo 3,110, tangu ugonjwa huo uliporipuka mwaka jana.

Ugonjwa huo umeshasababisha vifo vya watu 77 nchini Iran ndani ya kipindi cha wiki mbili, idadi ambayo ni kubwa zaidi nje ya China.

 

Babu wa Loliondo aibuka na utabiri mpya
Gwajima mbaroni kwa uchochezi akitumia Kisukuma