Mchungaji Ambilikile Mwaisapile maarufu kama Babu wa Loliondo, amedai kuwa Mungu amemuonesha utabiri mwingine kwamba, litatokea tetemeko kubwa la ardhi muda wowote na sehemu yoyote duniani, na litadumu kwa masaa manne, lakini halitoweza kuleta madhara yoyote.

Amesema kuwa licha ya idadi ya watu wanaofika kijijini hapo kupungua kwa ajili ya kunywa kikombe chake, lakini huduma yake bado inaendelea.

Ameongeza kuwa  kwa idadi ya watu wanaofikia kupata kikombe Mchungaji Ambilikile amesema kunachangiwa na uvumi uliopo kuwa Babu wa loliondo alishafariki huku baadhi ya watu wakionekana bado wakiendelea kufurahia huduma ya kikombe.

“Nimeelezwa na Mungu habari ya tetemeko kubwa, ambalo linakuja na halina madhara, hakuna mtu atakayekufa wala nyumba kuanguka, hata likija usiku mvua inanyesha watu wasikimbie kwenda nje litatikisa masaa manne, kuanzi saa 6:00 na litakata saa 10:00 usiku” amesema Babu wa Loliondo.

Mchungaji Mwasapile amesema kwamba Tanzania inaenda kuwa kioo na taifa la mfano ambapo mataifa mengi kote duniani yatafika hapa nchini kujifunza mambo mbalimbali.

Ikumbukwe kwamba kati ya mwaka 2010 na mwaka 2011 huduma ya kikombe cha babu ilivuta maelfu ya watu kutoka kila kona ya nchi kwa kile kilicho aminika kutibu maradhi sugu ya mwili.

Biden afungua jumanne maalumu ya ushindi
Wafungwa 54,000 waachiwa kwa hofu ya virusi vya Corona