Zaidi ya wafungwa 600 katika Gereza la Kuje nchini Nigeria, wametoroka wakitumia mwanya wa shambulio la kigaidi, linalodaiwa kufanywa na waasi wa Boko Haram ambapo Askari wawili waliuawa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Nigeria, Dkt. Shuaib Belgore amesema washambuliaji hao wa Boko Haram walikuwa walifikia Gerezani hapo mahsusi kwa ajili ya kuwatoa wanachama wao waliozuiliwa.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Belgore alikiri kwamba Wakala wa Kikosi cha Usalama na Ulinzi wa Raia wa Nigeria NSCDC, aliuawa katika shambulio hilo na kudai kuwa bado wanawatafuta wafungwa hao.

Hali ilivyokuwa mara baada ya kutekelezwa kwa shambulizi la Gereza la Kuje nchini Nigeria

“Kumekuwa na mashambulizi kadhaa kwenye vituo vyetu vingi vinarudishwa nyuma, lakini kila kukicha kuna moja ambayo wamefanikiwa katika hili ni moja walikuja kuamua sana na milipuko ya juu,” amesema Dkt. Belgore.

Ameongeza kuwa, Jaribio la awali la kuingia katika Greza hilo halikufaulu na kwamba baadaye wakashambulia sehemu nyingine ya ukuta na vilipuzi vya viwango vya juu ambavyo viliangusha ukuta.

“Vikosi vilivyokuwa chini vilifanya kila wawezalo kuwafukuza lakini idadi waliyokuja nayo ilikuwa kubwa ambayo hawakuweza kupambana nayo,” amengeza Katibu Mkuu huyo.

Wanachi wakiwa katika taharuki mara baada ya Boko Haram kuvamia na kulipua Gereza la kuje nchii Nigeria na wafungwa 600 kukimbia.

Aidha, amesimulia kuwa Wanamgambo hao waasi waliendelea kupigana na kwa bahati mbaya uvunjaji milango na maeneo kadhaa ya kuta ukafanikiwa na kudai kuwa tayari ulinzi umeimarishwa katika eneo lote la Gereza.

Mbali na kifo cha Wakala wa Kikosi cha Usalama na Ulinzi wa Raia wa Nigeria, pia Boko Haram walimuua mhudumu mmoja wa NSCDC aliyekuwa akijaribu kuokoa hali ya utorokaji wa wafungwa wa Gereza hilo wapatao 994.

Ulinzi ukiwa umeimarishwa maeneo jirani na Gereza la Kuje nchini Nigeria mara baada ya shambulizi linalodaiwa kufanywa na Boko Haram.

Ahmed Ally ampigia kampeni Suma Mwaitenda
Suma Mwaitenda achukizwa Young Africans