Klabu ya Tottenham imeibuka na ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya West Ham United katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ‘EPL’ uliopigwa leo katika uwanja wa London Stadium.
Harry Kane ambaye yuko katika ubora wake amepachika mabao mawili ya haraka kipindi cha kwanza akifunga dakika ya 34 na dakika ya 38 na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa Tottenham kuongoza kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili Christisn Eriksen alifunga bao la tatu kwa Tottenham dakika ya 60 kabla ya mshambuliaji kutoka Mexico Javier Hernandez kuifungia West Ham bao la kwanza dakika ya 65.
-
Video: Atletico Madrid yaibamiza Sevilla
-
Messi, Ronaldo, Neymar kuchuana mchezaji bora wa FIFA
-
Huu ndio wimbo unaomkera Lukaku
Tottenham wakicheza pungufu baada ya Aurier kupewa kadi nyekundu walijikuta wakishambuliwa na West Ham na dakika ya 87 Cheikhou Kouyate aliipatia West Ham bao la pili. Vijana wa Mauricio Pochettino walilinda vizuri lango lao na kuibuka na ushindi wa 3-2 dhi ya West ham.
Baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2, Tottenham sasa wamefikisha pointi 11 baada ya kucheza michezo 6 huku Wst Ham wakiwa na pointi 4 baada ya kucheza michezo 6 pia.