Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendelea kutoa huduma ya kupandikiza figo ambapo hadi hivi sasa tayari wagonjwa 19 wamenufaika na huduma hiyo tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini Novemba mwaka 2017.
Utoaji wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambayo ili elekeza kuweka mipango thabiti ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Aidha, taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Prof. Lawrence Museru kuhusu upandikizaji figo.
-
Polisi wajipanga kuhakikisha usalama siku ya Sikukuu ya Eid el Hajj
-
Habari Picha: Marais Wastaafu kuungana Rais Dkt. Magufuli kwenye mazishi
-
Habari Picha: Rais Dkt. Magufuli aongoza mamia ya watu katika mazishi ya Dada yake
“Tunapenda kuwafahamisha kuwa wagonjwa wote tuliowapandikiza figo pamoja na ndugu zao waliojitolea figo wanaendelea vizuri na shughuli zao kama kawaida. hii inaonesha ni kwa kiwango gani huduma hii imefanikiwa tangu ilipoanzishwa Novemba mwaka jana,” amesema Dkt Swai.