Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza kuongezeka kwa watu 53 wenye maambukizi ya virusi vya Corona idadi ambayo imepelekea kuwa na jumla ya visa vya corona nchini Tanzania kufikia 147.

Ambapo wagonjwa 38 wanatoka Dar es salaam, 10 Zanzibar, mgonjwa mmoja kutoka Kilimanjaro, mmoja kutoka Mwanza, mmoja Lindi na mwingine mmoja kutoka Kagera.

Takwimu hizo zimetolea baada ya saa 24 zilizopita kutangazwa idadi ya wagonjwa 6 kutoka Zanzibar.

Waziri Ummy amesema tangu machi 16, 2020 ni watu pekee 11 walipona dhidi ya virusi hivyo huku kukiwa na vifo vya watu watano.

”Serikali imeamua rasmi kwamba Hospitali ya Rufaa ya mkoa Amana ndio itatumika kama kituo maalumu cha matibabu cha wagonjwa wa Covid 19 lengo la serikali ni kuilinda hospitali ya Taifa Muhimbili dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona”amesema Ummy

Aidha amewataka wananchi ambao wanadalili za Corona wasiende hospitali ya Muhimbili na kwenda kwenye Hospitali zilizotengwa na serikali kwa aajili ya kutibu wagonjwa wa Corona.

Italia: Waathirika wa Corona kutambuliwa kwa simu
Wachezaji Arsenal kulimwa mishahara