Taasisi ya Vijana Wenye Ulemavu (YOWDO), imetoa mafunzo maalumu kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kuhusu namna bora zaidi ya kuripoti habari kwa kuzingatia watu wenye ulemavu

Akitoa mafunzo hayo mkuu wa programu ya mafunzo wa taasisi hiyo, Genarius Ernest amesema matumizi ya lugha zisizofaa zinazotumika kuwatambulisha watu wenye ulemavu ni miongoni mwa makosa ya mara kwa mara yanayofanywa na vyombo vya habari bila kujua na kusababisha hisia za unyanyapaa na karaha kwa watu wenye ulemavu

Mkurugenzi Mtendaji wa @yowdo_tanzania Rajab Mpilipili amesema ni muda sasa wa Jamii kubadilika na kuacha vitendo vya ubaguzi na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu ikiwemo tabia ya kuwachukulia kuwa ni watu wa kundi maalumu.

Mafunzo hayo ya siku moja ni sehemu ya mkakati wa @yowdo_tanzania wa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapewa nafasi sawa kwenye jamii na vyombo vya habari nchini, Mpango uliopewa jina la “ZAMU YANGU KUONGEA”

Dkt. Gwajima: Ukeketaji umepungua Tanzania
'Paracetamol' yatumika kuua nyoka