Je wajua dawa ambayo tunatumia kupunguza maumivu, Paracetamol pia ni dawa ya kuua nyoka? Basi kama bado washangazwa na hilo, nchini Marekani dawa hiyo inatumika kuua aina ya nyoka ambao ni ‘Brown Tree Snake’ katika kisiwa cha Guam.

‘Brown Tree Snake’ ni nyoka wenye urefu wa mita tatu ambao huishi kwenye miti na hula panya walionaswa kwenye magamba ya miti na inahofiwa kwamba idadi ya nyoka hao imeongezeka mara dufu katika kisiwa cha Guam.

Brown Tree Snake

Serikali ya Marekani hutumia miligramu 80 ya paracetamol, kwa kuwapa panya kama mtego ambapo wanapokula dawa hiyo huua nyoka baada ya dakika chache.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Kilimo ya Marekani, mbwa wa kunusa hutumiwa katika kuwatambua nyoka hao na ili kuthibitisha kuwa nyoka wameuawa na paracetamol, wao hutumia vifaa maalum kufuatilia baadhi ya panya.

Serikali ya Marekani ambayo inatakiwa kulinda wanyama pori imeamua kuwaua nyoka hao kwa sababu ya uharibifu unaofanywa na nyoka hao ikiwa ni tishio kwa aina ya ndege wa kipekee ambao ni nadra kupatikana na inadaiwa kwamba aina tisa ya ndege hao wa kipekee kati ya 11 wameangamia kutokana na kushambuliwa na nyoka hao.

Inatajwa kuwa nyoka huyo pia ni hatari kwa maisha ya twiga na popo, pia ndio chanzo cha kupotea kila mara kwa nguvu za umeme huku vikiharibu vifaa vya usambazaji wa umeme.

Kutokana na changamoto hizo ambazo hugharimu pesa nyingi kukabiliana nazo, serikali ya Marekani iliamua kutumia dawa ya paracetamol kudhibiti nyoka hao katika kisiwa cha Guam.

Wahariri wapigwa msasa habari za wenye ulemavu
Frank Komba kumsaidia Tesema Ligi ya Mabingwa Afrika