Mwamuzi wa Kimataifa wa Tanzania Frank John Komba amepangwa kuwa Mwamuzi msaidizi wa mchezo wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kati ya Raja Casablanca ya Morocco dhidi ya Amazulu ya Afrika Kusini.

Komba mwenye Beji ya FIFA ambaye alikua sehemu ya waamuzi walioteuliwa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika 2021 ‘AFCON 2021’ zinazoendelea nchini Cameroon, ataongozwa na Mwamuzi wa kati kutoka Ethiopia Tesema Weyese.

Waamuzi wengine katika mchezo huo utakaopigwa Jijini Casablanca (Morocco) kwenye uwanja wa Mohammed V Complex Februari 12, ni Mohammed Abdallah Ibrahim wa Sudan atakayekuwa msaidizi namba 1 na Mahmoud Ali Mahmoud Ismail wa Sudan atakayekuwa mezani.

Fursa hiyo ni kubwa kwa Mwamuzi wa Tanzania Frank Komba, kwani ameteuliwa kufanya kazi na Mwamuzi Tesema ambaye ni mmoja ya waamuzi bora Barani Afrika kwa sasa, wanaopigiwa chapuo kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia la FIFA zitakazounguruma nchini Qatar baadae mwaka huu.

'Paracetamol' yatumika kuua nyoka
Uchaguzi Kenya 2022: Kalonzo, Odinga kuungana, Ruto apotea