Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chamwino, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Grace Salia amewataka wanafunzi wanaomaliza elimu ya Sekondari kutokujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwani kufanya hivyo ni kutengeneza kizazi cha uhalifu.

Grace aliyasema hayo alipokuwa akiongea na wanafunzi wa kidato cha Nne shule ya Sekondari Maira mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwaeleza madhara ya kukaa kijiweni bila kuwa na kazi jinsi yanavyo pelekea kujiingiza kwenye uhalifu.

Amesema, “jiepusheni na vitendo vya kiuhalifu, kukaa kijiweni pia muepuke kwani ukikaa kijiweni bila kazi kuna madhara na hatari za kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa, epukeni makundi mnayoona si mazuri kitabia.”

Katika hatua nyingine, SSP Salia aliwaeleza wanafunzi hao namna ya utoaji taarifa za uhalifu na wahalifu, ikiwa ni pamoja na utoaji taarifa za ukatili wa kijinsia.

Makala: Vyombo vya Habari suluhisho ukatili wa Mtandaoni
Uchaguzi DRC: Wagombea kuanza rasmi kampeni leo