Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa leo augost 24,2020 amesaini sheria inayozuia wanafunzi wa kike nchini humo kukatishwa masomo pindi wanapopata ujauzito, hatua hiyo imekuja baada ya uwepo wa ugumu kwa wasichana kuendelea na masomo.
Sheria hii imekuwa na uungwaji mkono wa watu wengi wakidai, inatoa nafasi sawa kwa wanafunzi wa kike na wa kiume kuweza kumaliza masomo na kutimiza ndoto bila kuwa na vikwazo vyovyote vya unyanyasaji wa kijinsia.
Nchini Zimbabwe huenda hali hii ingekuwa tishio kwa wasichana wengi kukosa masomo yao kabla ya kuidhinishwa kwa sheria hiyo ambayo inakomesha matumizi ya bakora kwa lengo la kuwaadhibu wasichana wajawazito wawapo shuleni.
Tangu kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona, mwishoni mwa mwaka 2019 nchi nyingi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara zimeshuhudia idadi kubwa ya watoto wa kike wakipata ujauzito kipindi cha likizo.