Wakaazi wa eneo la Chuini, Unguja wamepinga agizo la Serikali kupitia Kamisheni ya Ardhi visiwani humo la kuvunja nyumba zao.
Wamesema kuwa licha ya kukaa kwa miaka mingi katika eneo hilo, wamewekeza kwa hali na mali. Hivyo, wamedai hatua ya kuondolewa katika maeneo hayo inawapa wakati mgumu kwakuwa hawana maeneo mengine ya kuishi.
Aidha, wametaja kutozifahamu sheria zinazotumika kuwaondoa katika eneo hilo kuwa ni moja ya changamoto zinazowaingiza kwenye matatizo hayo.
“Sheria ziko kwenye vitabu lakini sisi wananchi wa kawaida hatuzijui,” alisema mkaazi wa eneo hilo, Rashid Ramadhani ambaye hata hivyo alikiri kuwa nyumba zao zimejengwa kiholela.
“Lakini tunaomba serikali itusaidie hasa ikizingatiwa kwamba tumetumia fedha nyingi za kiinua mgongo angalau tupate sehemu za kujihifadhi,” aliongeza.
Naye Mwanasheria wa Kamisheni ya Ardhi visiwani Zanzibar, Hassan Nassor, amesema kuwa taratibu zote za kisheria zimefuatwa kabla ya kufikia uamuzi huo.
-
Nimechukuliwa na CCM kwasababu mimi ni jembe- Diwani Elirehema
-
Video: Masauni awaonya wanaotaka kuandamana
“Uhakiki wa eneo hilo umeshafanyika, na unaonyesha kwamba wengi wao hawana vithibitisho vya kisheria vinavyowaruhusu kutumia eneo hilo,” Nassor anakaririwa na kituo cha runinga cha Azam.
Aidha, Nassor ametoa wito kwa wananchi kufanya jitihada za kuzifahamu sheria na kujua matumizi sahihi ya ardhi ili kuepuka migogoro, hasara na usumbuf.