Baadhi ya mashabiki wa timu ya Ndanda wamelalamikia uongozi wa klabu hiyo kwa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi huku wakidai kuwa uongozi huo umekurupuka.

Mashabiki hao wamesema ni vema uongozi ungesubiri  ligi imalizike kwani kwa sasa siyo kipindi kizuri na kuna hali ya taharuki kwa mashabiki wa timu hiyo.

Wengi wa mashabiki hao wameoneshwa kukerwa na kitendo hicho huku wakimtupia lawama katibu mkuu wa wa klabu hiyo Kunyangana Njowoka, wakimtuhumu kujitokeza pindi timu yao inapocheza na timu kubwa pekee.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mashabiki wa timu hiyo Ismaili Ngalumbana amepingana kundi la wenzake akisema kuwa huu ni wakati muafaka wa kufanya mabadiliko hayo na kufanya hivyo ni hatua iliyotukuka.

Bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Ndanda FC yenye maskani yake mkoani Mtwara Jumanne wiki hii ilitangaza kufanya mabadiliko madogo katika benchi lao la ufundi kwa kumuweka pembeni kocha msaidizi wa timu hiyo, Hamim Mawazo.

Uchebe, Shilole wazungumzia kuvunjika kwa ndoa yao
Wakazi wa Chuini Unguja walalamikia agizo la kuvunja nyumba zao