Imebainika kuwa jiji la Dar es salaam limekuwa kinara wa lugha chafu na matusi, pamoja na kuwepo kwa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 lakini bado haisadii, huku jiji la Mwanza likiongoza kwa wizi wa mtandaoni.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, ACP Barnabas Mwakalukwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, amesema kuwa jumla ya matukio 327 ya matusi ya mtandaoni yalilipotiwa kuanzia januari hadi juni mwaka huu.

Mwakalukwa amesema kuwa makosa hayo hasa yanatokea katika Wilaya ya Temeke huku akiweka wazi kuwa takwimu hizo zinaonyesha kupungua kwa matukio ya aina hiyo ikilinganishwa na mwaka jana ambapo matukio yaliyoripotiwa yalikuwa 911 ambako wilaya ya kinondoni iliongoza kwa matukio ya kutoa lugha chafu na matusi.

Aidha, katika mkutano huo uliokutanisha Uongozi wa Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na Kamati ya Ardhi ya Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar amesema kuwa jumla ya matukio 1,663 ya wizi wa fedha kwa njia ya mtandao yaliyoripotiwa ambapo Mwanza ilionekana kuwa kinara.

Hata hivyo, kwa upande wake, Naibu wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani ametoa onyo kali kwa wanaofanya uharifu wa njia ya mtandao na kusema kuwa hawapo salama na ameahidi kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria.

 

UN yatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano Syria
Video: Ndugai atoboa siri Maalim Seif kukwama, Mkemia mkuu kitanzini