Wakenya takribani 18 wamefariki nje ya nchi yao kutokana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu covid -19 tangu ulipoanza kuenea duniani.

Hayo yamebainishwa na katibu wizara ya mambo ya nje nchini humo, balozi Zacharia Kamau na kubainisha kuwa hadi sasa kuna mgonjwa mmoja wa covid 19 ambaye yupo chini ya uangalizi maalum ICU nchini Sweden.

kwamujibu wa Citizen tv, familia ambazo zitahitaji kurudisha miili ya ndugu zao zitatakiwa kugharamia usafiri na kwa zitakazoshindwa miili ya ndugu zao itazikwa kwenye aridhi za ugenini.

Aidha ametangaza kuwa wakenya 500 ambao wamekwama China na India kwasababu ya mlipuko wa homa kali ya mapafu covid -19, wataanza kusafirishwa wiki ijayo kwa nauli zao wenyewe.

Amesema kuwa kati ya watakao safirishwa 300 watatoka India na 200 watatoka China na watatumia ndege ya Kenya Airways.

Balozi Kamau abainisha kuwa watakaotoka India watarudishwa Kenya Mei 4 huku watakaotoka China waturudishwa Mei 8 mwaka huu.


Pluijm awakumbusha Young Africans misingi ya usajili
Visa vya Corona vyafika milioni 3 duniani