Hifadhi ya wanyama kaskazini mashariki mwa Kenya imethibitisha kuwa twiga wawili wameuawa ambao ni jamii ya chotara, Twiga hao walionekana mara ya mwisho kaunti ya Garissa miezi mitatu iliyopita.

Usimamizi wa hifadhi ambayo twiga hao walionekana kwa mara ya mwisho unaamini kwamba wawindaji haramu ndio waliohusika kwa mauaji ya twiga hao.

Mwaka 2017, Twiga chotara aligunduliwa na kuwa kivutio kikubwa katika hifadhi ya Jamii ya Ishaqbini Hirola ambapo Agosti mwaka jana alizaa watoto wawili.

Kufuatia vifo hivyo, dume (Mmoja wa Watoto) aliyezaliwa na twiga huyo anabaki kuwa twiga mweupe pekee vifo vyao vimepokelewa kwa masikitiko makubwa na watafiti pamoja na watoa huduma za utalii.

Aidha wanasayansi wanasema hali yao ya kuwa kama chotara kunasababishwa na seli za ngozi yao kutokuwa na rangi, hali hiyo ni tofauti na hali ya kuwa albino kwasababu wanyama huendelea kuwa na rangi nyeusi katika tishu zao laini.

Ikumbukwe kuwa hili ni pigo jingine katika juhudi za uhifadhi wanyama nchini Kenya mwaka jana vifaru 10 weusi wa kipekee walikufa kwasababu ya sumu ya chumvi wakati wa zoezi la kuwahamisha.

Twiga weupe walianza kugonga vichwa vya habari kwa mara ya kwanza miaka mitatu iliyopita pale wawindaji haramu walipowabaini, na video ikasambaa kwenye mtandao wa Youtube.

 

 

 

CCM watinga Segerea kumtoa Mashinji
Video: Undani wa hukumu ya kina Mbowe, Membe ahoji mchakato kufukuzwa kwake CCM