Wanachama wa Chama cha mapinduzi CCM, wakiongozwa na katibu wa itikadi na uenezi Humphrey Polepole, leo Mchi 11, 2020 wamefanikiwa kumlipia faini ya sh. milioni 30, mwanachama wao mpya dkt. Vicent Mashinji na wameongozana kwenda Gereza la Segerea ili kukamisha utaratibu wa kumtoa.

Akizungumza leo mara baada ya kukamilisha taratibu za Mahakama, Polepole amesema wana CCM walianza kuchanga jana jioni na wamelipia leo na kupata muhuri wa Mahakama hivyo hatua iliyobaki ni kumtoa gerezani.

” Leo asubuhi tumefika hapa, tumefanikiwa kufuata taratibu za kimahakama, tumepewa ‘control’ namba na tumelipa benki, tumepewa lisiti yenye muhuri mbichi, tunakwenda segerea kumchukua ndugu yetu” amesema Polepole.

Mashinji pamoja na viongozi wengine 8 wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jana walihukumiwa kulipa faini ya milioni 350 au kifungo cha miaka 5 jela kwa kukutwa na hatia ya kesi ya uchochezi na waliposhindwa walipelekwa gereza la segerea.

Waziri wa Afya Uingereza akutwa na Corona
Wakenya waomboleza mauaji ya Twiga weupe