Wakimbizi raia wa Burundi wameanza kuitikia wito uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alioutoa akiwa zirani mkoani Kagera wa kuwataka warudi nchini kwao kwa hiari.
Kufuatia hatua hiyo, Mkutano wa pande tatu utakaojumuisha Serikali za Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) unatarajiwa kufanyika mwishoni wa mwezi huu kujadili namna ya kuwarejesha nchini mwao wakimbizi hao kwa kuzingatia sheria za kimataifa zinazohusu wakimbizi.
Aidha, Mkurugenzi Idara ya Huduma za Wakimbizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke amesema kuwa tangu kutolewa kwa wito huo, Wizara imekuwa ikiwamahasisha wakimbizi hao wa kujiorodhesha kwa hiari ili waweze kurejea nyumbani.
Mseke amesema kuwa hivi sasa kuna wakimbizi raia wa Burundi 276,692 kati ya wakimbizi 348,019 walioko nchini, huku akisema wengine ni wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) 70,840, Wasomali 150, na wengine (mchanganyiko) 337.
“Mwezi Januari mwaka huu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alifuta tamko la Primafacie alilolitoa mwezi Mei, 2015 ambalo linataka wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini kwao waruhusiwe kuingia kwa makundi bila ya utambuzi,”amesema Mseke.
-
Halmashauri Rukwa zaonywa dhidi ya matumizi mabovu ya mashine za EFD
-
PPF yawakumbuka wananchi wa Mafinga
-
Video: Jeshi la Polisi Rukwa lakamata vito vya thamani vilivyopitishwa kimagendo
Hata hivyo, ameongeza kuwa, bila ya tamko hilo Rais Dkt. Magufuli Tanzania kwa wastani ingekuwa inapokea wakimbizi 30,000 kwa mwezi na hadi kufikia sasa tayari imeshapokea wakimbizi wapatao 240,000.