Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) umewezesha wakulima 17 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kukopeshwa zaidi ya shilingi Milioni 500 baada ya Vijana hao kurasimisha ardhi yao,

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi mara baada ya kukabidhi hati za haki miliki zaidi ya 300 kwa wananchi wa Kijiji cha Magubike Wilayani humo Mkoani Morogoro.

Amesema kuwa fedha hizo zilitolewa kwa wakulima wadogo wa mashamba ya Miwa kutoka Benki ya Maendeleo ya Wakulima Tanzania (TAB) ili waweze kupata fedha za kuwasaidia kulima kilimo ambacho ni bora zaidi na chenye tija.

“Mbali na Benki hiyo, Benki zote hizo zina madirisha ya kukopesha, ndani ya Wilaya ya Kilosa tunayo Benki ya CRDB inafanya kazi kama hizo lakini tunayo Benki ya AZANIA ambayo inatumia njia nyingine, imeanza kuonesha nia ya kuwakopesha, changamoto ilikuwa upatikanaji wa hati hizi za kimila, lakini nyingi zinaonesha nia ya kukopesha kama hati hizi zitaendelea kupatikana” alisema Mgoyi.

Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya ametumia nafasi hiyo, kuwataka wananchi kutoka vijiji 37 ambavyo tayari vimekwisha fanyiwa upimaji wa Ardhi na kuweka mpango Bora wa matumizi ya Ardhi, waliopata hati hizo siku za awali na wale waliopata siku hiyo, kutumia fursa hiyo ili kuondokana na umaskini waliokuwa nao.

Naye Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Seraphia Mgembe amewataka Wakurugenzi kuwasaidia wananchi wenye hati katika kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili wapate mikopo hivyo.

 

Shilole amkejeli Alikiba kiaina, 'kuna msanii yupo lakini hatuna faida naye'
Mbunge wa CUF amtaka JPM achukue maamuzi magumu