Serikali imetoa shilingi Bilioni tatu katika kituo cha utafiti TARI kwa mwaka wa Fedha 2020/21 ili kuongeza utafiti na uzalishaji wa mbegu bora za Mkonge zitakazogawiwa kwa wakulima kwenye mikoa 17 inayolima zao hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema lengo kuu ni kuona kituo hicho kinazalisha mbegu bora milioni tano ili zigawiwe kwa wakulima
Kusaya ameongeza kuwa lengo ni wakulima hao wazalishe Tani 120,000 ifika mwaka 2025 kutoka tani 36,000 zinazozalishwa sasa
Naye, Mkurugenzi wa TARI Beatrice Senkoro, amesema wameanza kutekeleza hilo kwa kuongeza eneo la kulima mbegu kutoka hekta mbili za sasa mpaka hekta 65.
Senkoro ameiomba Wizara ya kilimo kuendelea kukiwezesha kituo kuwa na maabara ya kisasa ili kuongeza kasi ya utafiti wa mbegu bora za mkonge kwa njia ya “Tissue Culture Laboratory.”