Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 18, 2023 amezindua Mradi wa Uzalishaji wa Mbegu za Mazao ya Kilimo Wilayani Nzega, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Mkoani Tabora.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameishukuru Wizara ya Maji chini ya Waziri wake, Jumaa Aweso kwa kuipatia Wizara ya Kilimo Bwawa la Maji la Kilimi na Bonde la Kilimo.

Bonde hilo lina ukubwa wa Ekari 1102 na lipo katika eneo la Uchama Wilayani Nzega litakalotumika kwa ajili ya kuanzisha Shamba hilo la Mbegu.

Bashe amesema, kuanzishwa kwa Shamba hilo la Mbegu linalosimamiwa na Wakala wa Mbegu Nchini (ASA) litachochea Mpango wa Serikali wa kuwawezesha Vijana katika Sekta ya Kilimo.

Lionel Scaloni: Messi bado yupo sana
Wanne wafikishwa Mahakamani kwa utakatishaji fedha