Wakulima wa Karafuu Visiwani Zanzibar, wanahitaji kuwezeshwa ili waweze kuzalisha zao hilo kwa wingi zaidi ili liweze kuwa na manufaa makubwa na bora zaidi kwa wananchi na taifa kwa jumla.
Hayo yamebainishwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman Kisiwani Pemba kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara ya chama hicho.
Amesema, “hivi sasa zao hilo limeongezeka thamani na kuwepo mahitaji makubwa katika nchi na Masoko mbali mbali dunaini, lakini uzalishaji wake umeshuka kutokana na kutowezeshwa vyema makulima ili waweze kuwa na juhudi ya kuwa ya kuzalisha kwa wingi na kunufaika na zao hilo.”
Aidha, Othman ameongeza kuwa, licha ya kuongezeka thamani na bei ya zao hilo, lakini uzalishaji wake unahitaji kufanyiwa juhudi za kuongeza kutoka tani kati ya tano na nene za sasa hadi kufikia 20 na kuweza kuinufaisha zaidi Zanzibar.