Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewatahadharisha Wakurugenzi wote watakaoshindwa kusimamia miradi ya maendeleo na wale wanaopenda
kukaa na fedha hizo bila kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa kuwa hatosita kuwachukulia hatua za uwajibishwaji kwa mujibu wa taratibu.

Mchengerwa ametoa tahadhari hiyo mara baada ya Serikali kusaini mikataba ya miradi ya kuimarisha huduma za barabara, masoko, vituo vya mabasi na daladala, bustani za mapumziko na burudani, mitaro ya maji ya mvua na vivuko vya maji, kwa Halmashauri 12 kwa awamu ya kwanza.

Amesema, “Wakurugenzi mnatakiwa kusimamia miradi iliyopo kwenye maeneo yenu na ikamilike kwa wakati kama mikataba inavyojieleza, ili kuondoa mianya ya rushwa na ubadhirifu. Katika eneo la fedha za miradi kumekuwepo na changamoto hata kwa TAMISEMI, ninaagiza mkalifuatilie mara moja, wakati mwingine fedha zinatumwa katika Halmashauri na majiji.’

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa.

Halmashauri hizo za majiji, manispaa na miji ni Arusha, Dodoma, Geita, Ilemela, Kahama, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Songea,
Sumbawanga na Tabora, zenye idadi ya watu wanaozidi 250,000 ikiwa ni kati ya makundi matatu yanayohusisha ujenzi wa barabara zenye
urefu wa kilometa 14,754 na mitaro 24.66 km kwa Dodoma, Kigoma, Kahama, Morogoro na Mbeya.

Mkataba huo ni sehemu ya Miradi ya uboreshaji miundombinu ya miji Tanzania – TACTICS, utakaotekelezwa kwa miaka sita kwa mkopo wa Dola 410 milioni sawa na Shilingi 984 bilioni toka Benki ya Dunia na lilishuhudiwa chini ya Wizara likihusisha Wakurugenzi wa Halmashauri, Wanasheria, Wakandarasi na Washauri wa Miradi
elekezi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mchengerwa ameagiza Kampuni ya Nyanza Roads Limited
isipewe mradi wowote mpya hadi itakapomaliza mradi ya awali iliyokadhibiwa na Serikali ambayo bado haijatekelezeka, licha ya kuwa Kampuni hiyo pia kusaini mradi wa ujenzi wa barabara zenye mtandao wa kilometa 12.8 kwa Halmashauri ya mji wa Ilemela wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini.

Nipo tayari kwa mazungumzo kumaliza vita - Jenerali Burhan
Sita kuzitapika Milioni 37.3 za makusanyo Halmashauri