Kufuatia Mkoa wa Dar es Salaam kufanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2016 kwa kuingiza shule 6 kati ya kumi zilizofanya vibaya, Ofisi ya Elimu Mkoa imewaagiza wakuu wa shule na wakurugenzi kutoa taarifa za kina juu ya sababu zilizopelekea kufanya vibaya.
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa, Janeth Nsunza alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha televisheni,amesema kuwa bado wanaendelea na kikao kujadili tathmini ya matokeo hayo na amesema watatoa taarifa kamili watakapomaliza majadiliano.
“Kati ya shule 10 ambazo hazikufanya vizuri shule hizo ni Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole, Somangila day na Kidete kufuatia shule hizo sita kutofanya vizuri mkoa wa Dar es Salaam, umepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani imekuwa ni kinyume cha matarajio yetu na serikali yetu kwa ujumla.”amesema Nsunza.
Hata hivyo amesema Kwakuwa matokeo yameshatanganzwa, hatua zimechukuliwa ili kufahamu kwanini hali hiyo imejitokeza ambapo wahusika wanaendelea kutoa maelezo yao licha ya kuwepo kwa viashiria katika mtihani wa Mock na wakurugenzi waliwaelekeza wakuu wa shule hizo kuondoa hali hizo mapema.