Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi, amewataka Wakuu wa upelelezi Mikoa  kuhakikisha wanawalinda wananchi  katika masuala ya uhalifu wa kimtandao.

Ameysema hayo leo Machi 21, 2022 wakati wa ufunguzi wa wa mafunzi ya makosa ya mtandao (cybercrime) huku akiwataka wakuu hao kutumia mafunzo hayo katika kukabiliana na masuala ya uhalifu wa kimtandao kwa kujifunza zadi kuhusiana na masuala hayo ili wawe wabobezi.

Aidha Walioshiriki mafunzo hayo ni Askari 100 kutoka Jeshi la Polisi wakiwemo Wakuu wa Upelelezi  Mikoa, pamoja na vikosi,wakuu wa madawati ya  upelelezi wa Makosa ya  mtandao wa Mikoa na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Polisi.

“Nimefurahi tumekuja kujifunza jambo muhimu,tuliopo hapa tumekuja kupata elimu kwa wataalamu halisi dunia yetu inabadilika  sana mfano sasa hivi ugomvi wa Urusi na Ukraine  na mnafahamu pamoja na vita lakini ipo vita ya kidigital na uhalifu sio wa ndani pekee.Unaweza ukatendwa kwa kukusudiwa au kwa  kutokukusudiwa,”amesema.

Amesema mafunzo hayo  ni muhimu kwani yanawaonesha  nini wanatakiwa kufanya katika usalama wa Nchi  na raia

Naye,Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya  jinai nchini,Kamishna Camilius Wambura( DCI) amesema mafunzo hayo yanahusisha washiriki 100 kutoka Jeshi la Polisi wakiwemo Wakuu wa Upelelezi  Mikoa, pamoja na vikosi,wakuu wa madawati ya  upelelezi wa Makosa ya  mtandao wa Mikoa na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Polisi.

Rais Zelensky: vita imewageuza raia kuwa mashujaa
TBS yatoa elimu kwa wahariri