Shirika la Viwango Tanzania TBS limetoa wito kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kutumia kalamu zao vizuri katika kufikisha habari zilizo sahihi katika jamii.

Akizungumza na wahariri hao leo Machi 21, 2022 katika Ofisi za TBS Makao makuu Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS Viola Masako amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kumuelimisha muhariri majukumu ya TBS na kazi zake Ili atumie kalamu kuelimisha jamii.

“Kwa kuwaelimisha wahariri shughuli mbalimbali zinazofanya na shirika la TBS
kwani wahariri ndo jicho la taifa, mtakachokwenda kuongea, mtakacho elimisha jamii ndicho kitakachopokelewa, ” Amesema Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS Viola.

Aidha mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo umuhimu wa ushiriki katika mchakato wa uandaaji viwango, Huduma zitolewazo na kuruhenzi ya upimaji na Ugezi.

Meneja Viwango shirika la viwango TBS Yona Afrika akizungumza mbele ya mkutano wa Wahariri vyombo vya habari akitoa mada ya umuhimu wa ushiriki katika mchakato wa uandaaji viwango

Wakuu wa upelelezi wapewa maagizo
Ujenzi wa mzani kemondo wapandisha mapato