Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ametoa rai kwa Wakuu wa Wilaya hapa nchini kuzingatia utawala bora, kanuni, sheria na utaratibu katika uongozi na utatuzi wa migogoro katika maeneo yao.
Dkt. Mpango ameyasema hayo leo hii leo Machi 13, 2023 wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba.
Amesema ni vema viongozi hao kuzingatia maadili ikiwemo kudhibiti uvujaji wa siri za serikali kwa kujiepusha na matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii pamoja na barua pepe binafsi katika kutuma nyaraka za serikali.
Pia ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya kuzingatia utaratibu katika matumizi ya walinzi binafsi na waandishi wa habari katika ofisi za umma.