Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Athumani Amasi amesema wanafunzi 2,095 kati ya 2,180 waliofanya mtihani wa marudio wa darasa la saba uliofanyika kati ya Desemba 21 na 22 mwaka 2022 wamefaulu daraja A hadi C sawa na asilimia 96.1.
Wanafunzi hao kati ya 2,194 waliofutiwa matokeo ya mtihani huo na Necta baada ya kubainika kufanya vitendo vya udanganyifu uliofanyika Oktoba 5, 6 mwaka 2022.
Amasi amesema kati ya wanafunzi 2,194 waliofutiwa matokeo waliofanya mtihani 2,180, wachache hawakushiriki mchakato huo kwa sababu mbalimbali, akisema huenda wengine walikwenda nje ya nchi.
Mitihani wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika Oct/November 2022 ambapo kwa upande wa darasa la nne Wanafunzi 1,320,700 kati ya 1,592,235 wenye matokeo sawa na 82.95% wamefaulu.
Kwa upande wa kidato cha pili, Jumla ya wanafunzi 539, 645 kati ya 633, 537 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 85.18 wamefaulu madaraja ya I, II, III na IV.