Shirika lisilokuwa la Kiserikali la We are all needed (WAN) limepongeza hatua iliyochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kukataza wanafunzi wenye ujauzito kuendelea na masomo katika shule za Serikali.
Hayo yamesemwa mapema hii leo na jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Shirika hilo, Salome Lwena alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuunga mkono agizo hilo.
Amesema kuwa shirika lake liko tayari kumuunga mkono Rais Magufuli katika harakati za kukuza na kuendeleza maadili nchini ikiwemo suala la kupunguza mimba za utotoni kitu ambacho kitasaidia jamii kuwa makini.
“Sisi WAN tunaunga mkono kauli ya Mh. Rais kuhusu suala la ukatazaji mimba kwa shule za Serikali za Msingi na Sekondari ili wanafunzi hao wasiathiri wanafunzi wengine kwani wanafunzi wakipata ujauzito wanaathirika kisaikolojia,”amesema Lwena.
Ameongeza kuwa kauli ya Rais Magufuli imewapa nguvu ya kuzidi kutoa elimu ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi ili wasome hadi watakapokamilisha ndoto zao kwani linajihusisha na shughuli ya kutoa elimu ya kujitambua kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini.
-
Serikali kuimarisha uhusiano na vyombo vya habari nchini
-
Dkt. Mpango awaonya wanaokwepa mashine za EFDs
-
Wananchi kunufaika na mradi wa maji ya Ziwa Victoria
Hata hivyo, kwa upande wake Katibu wa shirika hilo, Romanus Dominicus ametoa wito kwa wazazi na walezi kuendeleza maadili katika Taifa kwani hakuna Taifa lililoendelea Duniani kwa kuharibu maadili na nidhamu ya watoto.