Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 1.669 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya ya Ileje mkoani Songwe.

Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Itumba.

Amesema kati ya fedha hizo sh. bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika miji miwili ya Isongole na Itumba wilayani Ileje. “Kiasi kingine cha sh. milioni 669 kimetengwa kwa ajili ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ileje katika mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Hata hivyo, amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa Kampeni ya Rais Dkt. Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma ya maji kwa urahisi.

Majaliwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400.

Pia, Majaliwa ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe kuhakikisha inaimarisha ulinzi katika maeneo ya mipaka. amesema kamati hiyo inatakiwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipaka ili kuizua wageni kuingia bila ya kufuata taratibu zilizowekwa kisheria.

 

Serikali kutoa chanjo ya Homa ya Ini kwa gharama nafuu
WAN yampongeza JPM dhidi ya hatua anazochukua