Wanafunzi 14 wa Shule ya Sekondari Rulongo Wilaya Muleba Mkoani Kagera, wamelazwa katika hospitali ya Rubya baada ya kujeruhiwa na radi iliyoambatana na mvua yenye upepo mkali na kati yao wanafunzi watatu wanatajwa hali zao ni mbaya kiafya.
Mganga mkuu wa hospitali ya Rubya wilayani Muleba, George Kasibante amesema kuwa wanaotajwa kuwa na hali mbaya wameungua sehemu mbalimbali za miili yao na mwingine mmoja amepoteza fahamu na kwamba madaktari wanafanya liwezekanalo kuokoa maisha ya wanafunzi hao.
Amesema kuwa radi hiyo ilipiga vyumba vya madarasa, kidato cha pili na tatu ambapo baadhi ya wanafunzi walipatwa na mshtuko na shule hiyo imejengwa mlimani hivyo ni eneo ambalo matukio ya radi hutokea kwa sababu ya kuwepo miinuko kutokea ukanda wa mashariki
“Kawaida radi hupita sehemu yenye miti mirefu na majengo ya namna hiyo lakini tunaomba wazazi na walezi kuamini madakari kwa huduma zinazoendelea kutolewa, muhimu wanafunzi hawa wawaletee kadi za bima ya Afya” Amema Kasibante
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Muleba, Emanuel Sherembi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika shule ya Sekondari Rulongo kupigwa radi na kwamba amemtuma afisa elimu na mganga wa wilaya kufuatilia matibabu ya wanafunzi hao licha ya yeye kufika hospitalini hapo.
-
Baba Mzazi wa msanii wa bongo fleva Ali kiba Afariki Dunia
-
Kidato cha kwanza waruhusiwa kuvaa sare za shule ya msingi
-
Asasi za maendeleo zatakiwa kuwa chachu kwa vijana
Hata hivyo, Wilaya za Muleba na Ngara mkoani Kagera wakati wa mvua za vuli na masika mara nyingi sehemu zenye miinuko hukumbwa na matukio ya radi kila mwaka na kuleta madhara kwa watu na mifugo kupoteza maisha zikiwemo mali kadhaa kuharibika