Watu waliojihami kwa silaha nchini Nigeria, wamewateka Wanafunzi 35 wa chuo kikuu cha kilichopo eneo la Kaskazini-Mashariki mwa mji wa Zamfara, ikiwa ni tukio kubwa la utekaji linalowahusisha Wanafunzi ndani ya mwaka 2023 katika Taifa hilo.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Msemaji wa Gavana wa Zamfara, Mugira Yusuf, imeeleza kuwa takribani Wanafunzi 24, wafanyakazi 10 na Mlinzi mmoja walitekwa na watu wenye silaha mapema Ijumaa, kutoka chuo kikuu cha shirikisho cha Gusau.

Sehemu ya Wasichana wa Chibok waliookolewa baada ya kutekwa 2017. Picha ya Sunday Aghaeze/AFP.

Aidha, amesema magenge ya silaha yamekuwa yakishamiri katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, ambapo majaribio ya vikosi vya usalama kusitisha ghasia za makundi hayo yamekuwa na ufanisi mdogo. 

Hata hivyo, utekaji wa wanafunzi, ambao zamani ulikuwa unatumiwa na makundi ya wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu kuwatishia raia, umegeuka kuwa sekta ya kuchuma pesa na magenge ya uhalifu yanayoomba fidia.

Simba SC yashikilia kibarua cha Minziro
Fei Toto afunguka maisha ya Azam FC