Kenya jijini Nairobi Wanafunzi saba wa shule ya msingi Precious Talent wamethibishwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya baada ya darasa la shule yao kuporomoka leo asubuhi Jumatatu ya Septemba 23, 2019 muda mfupi kabla ya masomo kuanza.
Naye Mkurungezi wa shule hiyo ya kibinafsi, Moses Wainaina Ndirangu, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo alipozungumza na televisheni ya Citizen na kusema kuwa jengo hilo liliathiriwa na ujenzi wa bomba la maji taka unaoendelea karibu na hapo.
Shughuli ya kuokoa wanafunzi ndani ya darasa hilo inaendelea na baadhi ya wanafunzi wamekwama ndani ya darasa hilo.
Ambapo mafisa wa zima moto kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba mwekundu wanasaidiana na wenyeji kuwaokua watoto waliokwama chini ya jengo hilo.
Kamanda wa polisi, George Seda na mbunge wa eneo la Dagoreti, John Kiarie, wamethibitisha kuongezeka kwa idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wanasemekana kukimbilia makazi ya watu jirani na mtaa wa Dagoretti, Magharibi mwa Jiji la Nairobi baada ya jengo la shule kuporomoka.
Afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya elimu, Belio Kipsang, amewasili katika eneo la tukio.
Aidha, serikali imeanzisha uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo.