Wanafunzi wa darasa la saba Shule za msingi za Parknyigoti, Robanda na kote Nchiniambao wanatarajia kuhitimu elimu ya msingi wameaswa kutokukubali wala kujihusisha na mahusiano na ndoa za utotoni ambazo zitaharibu ndoto zao kielimu na kimaisha.

Wito huo umetolewa na Polisi kata ya Ikoma iliyopo Tarafa ya Grumet Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara, Koplo Emmanuel wakati akiongea na Wanafunzi hao na kuwataka pia kutoa taarifa pale wanapohisi au kufanyiwa vitendo vya kikatili huku akiwaelimisha kuhusu madhara yake.

Amesema, “msikubali kuolewa kabla ya umri sahihi, pia mtoe taarifa pale mnapohisi viashiria vya vitendo vya kufanyiwa ukatili au kama mmefanyiwa vitendo vya kikatili msikae kimya, ukimya una madhara na mtaharibu maisha yenu ya baadaye.”

Aidha, Koplo Emmanuel pia alitoa elimu ya kutojihusisha na vitendo vya kihalifu na uhalifu na badala yake wawe mfano mzuri katika jamii zao na kujikita zaidi katika kuwasaidia walezi na wazazi wao kazi za nyumbani na mashambani wakati wakisubiri matokeo ya Mtihani wao.

Lavia, Chukwuemeka wazua janga jipya Chelsea
Hali inazidi kuwa mbaya kwa Antony