Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Southern Highlands iliyopo Jijini Mbeya wameomba huduma ya vituo vya afya na Zahanati kuwapatia huduma ya kondom ili waweze kujinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi na zinaa.

Maombi hayo yamewasilishwa na mmoja wa wanafunzi Fotunatus Maseli (20) wakati wa utoaji wa elimu mbalimbali kupitia michezo na asasi isiyo ya kiserikali (YES TANZANIA)

Ambapo Msele amesema suala hilo limekuwa changamoto kwao kwani umri walionao unaruhusu kuhisi hisia hivyo inawabidi wafike kwenye vituo vya afya kuomba kupata huduma za kondom ambazo zinaweza kuwasaidia kujikinga na Ukimwi pamoja na mimba zisizotarajiwa.

Naye Lameck Mwilabu (21) mwanafunzi wa kidato cha sita amesema changamoto nyingine wanayokumbana nayo kama vijana ni kutopata ushirikiano kutoka kwa wahudumu wa afya pindi wanapohitaji kupima afya zao.

Clara Kibonde miaka 21 kidato cha sita katika shule hiyo amemuomba Waziri wa afya Ummy Mwalimu kushusha bei za taulo za kike ili kila mtu aweze kumudu gharama za taulo hizo, ameongeza kuwa wanaomba taulo za kike ziwe za aina moja kwani za kuvaa zina madhara hivyo wanaomba taulo za kufua ambazo wanaamini zina ubora.

Kwa upande wake Halima  Lila ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha Tumaini cha watoto, wasichana na wanawake Tanzania amesema karibu mikoa yote waliyotembelea changamoto zinafanana kwa kiasi kikubwa ambapo amsema changamoto kubwa ni mimba za utotoni na kuongeza kuwa sababu za kulenga vijana zaidi ni kutokana na wao kuwa na changamoto kubwa ni uwezo wa kuongea.

 

 

Video: Mapya yaibuka mtoto aliyeibwa na kichaa Mbeya, Bibi afunguka 'Watoto kuuzwa'
Polisi akatwa Nyeti na mkewe