Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Flora Adam (23), kwa tuhuma za kumkata mume wake sehemu zake za siri, ambaye ni Askari polisi aitwaye PC Kazimir (28), mkazi wa Shinyanga Mjini, kitendo ambacho kimeelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Deborah Magiligimba, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Disemba 28, 2019, majira ya saa 6:00 usiku, wakati wakiwa wamelala ambapo ghafla mwanamke huyo alinyanyuka kitandani na kumkata mume wake na kitu chenye ncha kali sehemu zake za siri.

Amesema wakiwa wamelala, ghafla Frola aliamka na kuanza kumnyatia huku akiwa ameshika kitu chenye ncha kali kisha kumkata mumewe sehemu za siri na kumjeruhi vibaya.

“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi ambapo mwanamke alikuwa akimtuhumu mume wake kuwa ananyumba ndogo, ndipo akaamua kuchukua kitu chenye ncha kali kisha kuanza kuukata uume wa mumewe na kumjeruhi vibaya”  amesema kamanda Magiligimba.

Baada ya tukio hilo Askari huyo, alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga, ambako alilazwa kwa siku mbili na badaye aliruhusiwa.

Aidha, kamanda huyo amesema jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke huyo na kwamba uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Wanafunzi waomba kupatiwa Kondom
Serikali yapiga marufuku mawakili nje ya ofisi za NIDA