Nibu waziri wa mambo ya ndani  ya nchi Mhandisi Hamad Masauni amepiga marufuku watu wanaojiita mawakili na kuwatoza wananchi kiasi cha  fedha kinachozidi shilingi Elfu Kumi  wakidai ni ada ya kupewa nyaraka mbadala ya cheti cha kuzaliwa ikiwa ni hitaji la msingi kwa wananchi wanaofika katika za NIDA

Amesema hayo akiwa makoani Morogoro baada ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Mkoa huo walioitaka Serikali kuweka bayana kama kupata vitambulisho vya taifa lazima ulipe hela, ambapo Naibu Waziri  amesema kuwa vitambulisho hutolewa bure hakuna haja ya kulipa gharama yoyote huku akipiga marufuku wananchi kutozwa fedha nje ya ofisi za NIDA.

“Kuanzia sasa kila Ofisi ya NIDA itakuwa na mawakili wa serikali wataohusika na kuandaa pamoja kuhakiki nyaraka mbalimbali za wananchi wanaokuja kwa ajili ya Vitambulisho vya Taifa.”amesema Masauni

Ameongeza, “Ninatoa maelekezo kwa nchi nzima katika Ofiisi za NIDA kuwaondoa watu wanaowaandalia wananchi nyaraka hizo kwanza hatuwatambui kama ni Maafisa Sheria Sahihi au la na wanaweza kuwathibitisha watu ambao sio raia wakapata vitambulisho kama raia”

Polisi akatwa Nyeti na mkewe
Papa Francis aomba radhi kwa kumpiga kibao mwanamke