Polisi nchini Nigeria, imesema inaendelea kuwatafuta watu wanaodhaniwa kuwa na Silaha wamewateka nyara Wanafunzi watano kaskazini mwa Taifa hilo, tukio ambalo linakuja siku chache baada ya wanafunzi wengine zaidi ya 20 kutekwa nyara katika eneo jirani ukanda huo.

Kupitia taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Msemaji wa Polisi wa Jimbo la Katsina, Aliyu Abubakar Sadiq amesema tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku, ambapo washukiwa hao wa ugaidi waliwateka nyara wanafunzi hao wa kike wa Chuo Kikuu cha Serikali.

Amesema, “ni chini ya wiki mbili tangu watu wenye silaha kutoka kwenye magenge ya uhalifu kuwateka nyara zaidi ya watu 30, wakiwemo wanafunzi wasiopungua 24 wa kike, katika uvamizi kuzunguka chuo kikuu kilichopo nje ya mji mkuu wa Gusau jimbo la Zamfara.”

Hata hivyo, tayari Wanajeshi wa Nigeria wamewaokoa mateka 16 wakiwemo wanafunzi 13 na utekeji nyara hio ni wa kwanza wa watu wengi katika chuo kimoja tangu Rais Bola Ahmed Tinubu aingie madarakani mwezi Mei, 2023 ambapo aliahidi kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini Nigeria.

Kesi ya uhujumu: Waziri Mkuu wa zamani anyimwa dhamana
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 6, 2023