Wanahabari wa Tanzania walioshiriki tuzo mbalimbali kutoka Merck Foundation tangu mwaka 2017/2022 wamekabidhiwa tuzo na vyeti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza April 2, 2023.
Akizungumza Mwenyekiti wa Merck Foundation Germany, Prof Frank Strangernberg amesema vyombo vya habari pamoja na wanahabari wanamchango mkubwa hasa kwa kuwasemea wale wasio na sauti na kuondoa mila na desturi potofu kwenye jamii.
”Kwa kutambua umuhimu wa wanahabari tumekuwa tukiwapatia mafunzo maalumu na tulianzisha tuzo kutambua mchango wao”
Mwenyekiti wa Merck Foundation Germany, Prof Frank Strangernberg
Kwa mwaka 2022 tumepata washindi nane kutoka Tanzania katika ukanda wa Afrika Mashariki wanne ni kwa upande wa Tuzo ya ‘more than a mother’ na wanne ni ile inayoangazia Diabetes & Hypertension” amesema Prof. Strangernberg
”Tunao pia washiriki wa Mwaka 2017, na wote walioshiriki hizi tuzo ninyi ni mabalozi wetu tunatambua mchango wenu katika kuangazia maswala yanayogusa afya ya jamii na kuleta mabadiliko”
Aidha amesema kuwa wanahabari wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kuelimisha jamii lakini pia kutokomeza unyanyapaa, kuhimiza elimu kwa watoto wa kike kutokomeza ndao na mimba za utotoni.
Prof. Strangernberg amesema Merck Foundation kwa mara ya kwanza iliweza kufanya mafunzo kwa njia ya mtandao kwa wanahabari watanzania kwa kushirikiana na Chama cha wanahabari wanawake Tanzania(TAMWA).
Ameongeza kuwa watatoa mafunzo kwa kushirikiana na baraza la Habari Tanzania MCT na Club ya waandishi wa habari Dar es Salaam (DCPC) imani yetu mtanufaika na mafunzo hayo na kuzidi kubobea zaidi katika upashaji wa habari.
Merck Foundation imekuwa ikitekeleza majukumu yake Barani Afrika kwa akushirikiana na wake wa Maraisi 20 barani Afrika kwa miaka 5 na kwamba yamepatikana mafanikio mengi katika kusaidia sekta ya afya na ustawi wa jamii.