Serikali nchini Zimbabwe, imewafungulia mashtaka wanaharakati 39 wa upinzani wanaoshutumiwa kuzua ghasia za kisiasa na kuharibu ofisi ya chama tawala siku ya Jumatatu (Juni 6, 2023), hali ambayo imeongeza mvutano kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.
Kwa mujibu wa Waendesha mashtaka wamesema, kundi hilo lilishambulia ofisi ya chama tawala cha ZANU-PF, ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1980 katika eneo la Nyatsime, kusini mwa mji mkuu, wiki iliyopita.
Aidha, kundi hilo linadaiwa kuharibu nyumba kadhaa na kuwashambulia watu wa jamii ya Nyatsime na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na kusababisha majeraha makubwa kwao, waendesha mashtaka walisema.
Hata hivyo, tukio hilo limekuja wakati makundi ya kutetea haki za binadamu na vyama vya upinzani nchini humo vikilalamikia kukandamizwa kuelekea uchaguzi mkuu. Mawakili wa watu waliokamatwa, hata hivyo, waliashiria kuwa mashtaka hayo yalichochewa kisiasa.