Wanaharakati 3 wa Haki za Binadamu wamehukumiwa kwenda jela miaka 10 kwa kutishia usalama wa taifa hilo kwa kufuatilia masuala mbalimbali.

Wanaharakati hao walikamatwa mwezi Juni mwaka 2017, wakiwa na nyaraka za maandalizi ya kongamano la wanaharakati wa Haki za Binadamu nchini humo.

Aidha, Watu hao wamefahamika kwa majina ya Emmanuel Nshimirimana, Aime Constant Gatore na Marius Nizigiyimana

Majaji katika mahakama ya Muramvya, walitangaza uamuzi huo bila ya uwakilishi kutoka kwa wanasheria wa washtakiwa, mwanaharakati ambaye aliomba kutotajwa jina.

“Hii ni mara ya kwanza katika historia ambapo wanachama wa kikundi cha kiraia nchini Burundi wamehukumiwa kwa njia hii” Gabriel Rufyiri, mwanaharakati maarufu nchini, amesema.

 

Rais aamua kujiuzulu kwa tuhuma zinazomkabili
Video: Dogo Janja amwimbia Uwoya ''Wayuwayu''