Makumbusho ya taifa la Tanzania iliyopo jijini Dar es salaam imeandaa mafunzo ya onyesho la chimbuko la binadamu Afrika yanayotarajiwa kutolewa kesho.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya taifa Prof. Audax Mabula, ambapo amesema mafunzo na onyesho hilo yanatokana na tafiti mbalimbali zinazofanyika bonde la hifadhi ya Olduvai na Laetol katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Amesema kuwa onyesho hilo litafanyika kesho jijini Dar es salaam na litafunguliwa na waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na litahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Hata hivyo, katika onyesho hilo wananchi pia wataweza kuona mambo mbalimbali ya kale ambayo binadamu wa kwanza aliweza kuyafanya katika nyanja tofauti katika maisha yake.